Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Michezo Samia aipa tano Yanga
MichezoTangulizi

Samia aipa tano Yanga

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga licha ya kutolewa na Mamelodi Sundowns katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya ligi ya Mabingwa wa Shirikisho la Soka Afrika. Anaripoti  Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika mchezo huo uliomalizika leo Ijumaa usiku, Yanga imeondolewa kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya dakika zote 90 zilizopigwa katika uwanja wa Loftus Versfeld jijini Pretoria nchini Afrika Kusini timu za Mamelodi Sundowns na Yanga kutoka sare tasa.

Aubrey Modiba of Sundowns challenges Mudathiri Yahya Abasi of Young Africans during the CAF Champions League 2023/24 quarterfinals 1st leg match between Young Africans and Mamelodi Sundowns at Benjamin Mkapa Stadium in Dar Es Salam, Tanzania on 30 March 2024 ©Weam MostafaBackpagePix

Gumzo katika mchezo huo ulioishia dakika 90 kwa 0-0 kama ilivyokuwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa wiki iliyopita, ni shuti la kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie  Aziz Ki dakika ya 58 ambalo liligonga mwamba wa juu  kwa ndani na kuvuka mstari wa chini ndani lakini teknolojia ya VAR ikainyima Yanga goli hilo.

“Kutokana na matukio ya mchezo huo, Rais Samia kupitia akaunti yake ya mtandao wa X ameandika hivi; Mchezo mzuri Yanga. Mmeonesha kiu na juhudi ya kuiletea heshima nchi yetu hadi kufikia hatua hii.

”Tunatarajia makubwa zaidi kutoka kwenu kwenye mashindano haya (Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika) msimu ujao. Tutaendelea kuwaunga mkono na kuwapa motisha.”

1 Comment

  • YANGA WANATAKIWA KUKATA RUFAA, HAIWEZEKANI GOLI LA WAZI NAMNA ILE LIKATALIWE!! AU KWA VILE NI MALI YA MOTSEPE NINI? HAYA MATOKEO YALIKUWA YAMESHAPANGWA KABISA. ILA KUKAA KIMYA NI MAKOSA LAZIMA DUNIA IONE NA KAMA NI UDHAIFU WA KANUNI BASI ZIFANYIWE MAREKEBISHO!! HAIWEZEKANI MECHI MUHIMU KAMA HIYO GOLI LIKATALIWE KIRAHISI TU!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

Habari za SiasaTangulizi

Haya hapa majina walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali CHADEMA

Spread the loveCHAGUZI wa kanda za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Uingereza yamwaga bil. 9 kumuunga mkono Samia matumizi nishati

Spread the loveWaziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani...

error: Content is protected !!