Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Samia ahesabiwa, “maswali sio magumu”
Habari Mchanganyiko

Samia ahesabiwa, “maswali sio magumu”

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amekuwa miongoni mwa Watanzania waliohesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza saa 6:01 usiku wa leo Jumanne tarehe 23 Agosti, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Samia amehesabiwa mapema leo katika ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na karani wa sensa ambaye awali alikuwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS), Albina Chuwa na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022, Anne Makinda.

Aidha, baada ya kumaliza kumhesabu, kazi iliyodumu si zaidi ya dakia 25, Rais Samia amesema, “nimemaliza kuhesabiwa, ni kweli maswali ni mengi kidogo lakini yanajibika, hakuna swali gumu.. ombi langu kwa wananchi ni kuweka taarifa zetu mapema.”

“Watu wa Takwimu, makamisaa walitoa maswali mapema, wananchi watafute hayo maswali ili waanze kutafutia majibu mapema.

“Mfano atauliza kama una bima ya afya, kadi ya NIDA namba ngapi, ukikaa nazo mkononi wanakwenda haraka. Kaya zetu wastani ni watu watano, kama hamkuwa tayari inaweza kuchukua muda mrefu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!