October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rosa Ree avishwa pete, amwaga chozi

Spread the love

 

MSANII wa Bongo Fleva, Rosary Robert maarufu ‘Rosa Ree’ amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, King Petrousse ambaye alimtambulisha kwa mashabiki zake hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rosa Ree ambaye muziki wake ni wa aina ya kufokafoka ‘Hip Hop’ mapema mwaka huu alianza kuwarusha roho mashabiki zake baada ya kufululiza kuachia picha za mpenzi wake huyo na kuwadhibitishia kuwa sasa mahaba yamekolea.

Kufuatia tukio hilo lililotokea jana tarehe 24 Septemba mwaka huu, baadhi ya mastaa na mashabiki wake wamempongeza kwa hatua hiyo.

Baadhi ya mastaa hao ni Mimi Mars, Amberlulu na wengine ambao wamemweleza kuwa anastahili kuvishwa pete.

error: Content is protected !!