October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

UVCCM: Tunakwenda na Rais Samia 2025

Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenan Kihongosi

Spread the love

 

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema vijana wa chama hicho wamekubaliana kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan hadi 2030. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 25 Septemba 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa UVCCM, Khenan Kihongosi, kwenye halfa ya kumpokea Rais Samia akitokea nchini Marekani kwa ziara ya kikazi.

“Sisi kama vijana wa UVCCM na vijana wote nchi nzima tunamuunga mkono na tumekubaliana kwamba kuanzia 2020 hadi 2025 na 2025 hadi 2030, tunakwenda na Rais Samia tena na tena, kuhakikisha anajenga nchi imara na umoja imara, vijana tuko pamoja naye,” amesema Kihongosi.

Licha ya kwamba Kihongosi hakutaja tukio maalum ambalo watakwenda na Rais Samia 2025 na 2030, katika miaka hiyo Tanzania inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Marekani, Kihongosi amesema itakwenda kufungua fursa za kiuchumi.

“Ziara yake hii ya kwanza nje ya Afrika inakwenda kufungua fursa za kiuchumi, sababu tumeona ameshakutana na wafanyabiashara mbalimbali, alienda na ujumbe wa wafanyabishara wetu wameenda kujifunza, fursa ni kubwa wawekezaji wengi watakuja, vikwazo vilivyokuwepo vimeondolewa, kwa hiyo wafanyabaishara watakuja kuwekeza,” amesema Kihongosi.

error: Content is protected !!