Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais wa zamani wa Angola Jose dos Santos afariki dunia
Kimataifa

Rais wa zamani wa Angola Jose dos Santos afariki dunia

Jose dos Santos
Spread the love

RAIS wa zamani wa Angola, Jose dos Santos, amefariki dunia leo Ijumaa, tarehe 8 Julai 2022, katika hospitali moja jijini Barcelona, nchini Uhispania, alikokuwa anapatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa ya kifo cha Santos aliyekuwa umri wa miaka 79, imetangazwa leo na Serikali ya Angola.,ambapo imesema alilazwa jijini Barcelona tangu Juni, mwaka huu.

Rais huyo wa zamani wa Angola, alilitawala taifa hilo linaloongoza kwa uzalishaji wa mafuta Afrika, kwa muda wa miaka 38, kuanzia 1979 hadi alijiuzulu 2017 kufuatia kuandamwa na kashfa ya rushwa.

Waziri wake wa Ulinzi, Joao Lourenco, alichukua madaraka baada ya Santos kujiuzulu.

Dos Santos atakumbukwa kwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu mwanzoni mwa miaka ya 2000 – wafuasi wake walimwita “mbunifu wa amani”.

Lakini urithi wake umechafuliwa na viwango vya juu vya ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu alipokuwa madarakani.

Akiwa amehitimu katika uhandisi wa petroli katika Umoja wa Kisovieti mwaka wa 1969, Dos Santos alikuwa na umri wa miaka 37 tu alipokuwa rais wa Angola muongo mmoja baadaye, kufuatia kifo cha rais wa kwanza, António Agostinho Neto.

Wakati huo, miaka minne tu baada ya kupata uhuru mwaka 1975, nchi hiyo ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi mawili yaliyokuwa yakipigania ukoloni wa Ureno – MPLA ya Dos Santos na Unita.

Vita hivyo vilidumu kwa miaka 27 na kuangamiza nchi. Takriban watu 500,000 wanaaminika kufariki katika mzozo huo.

Pia ilivutia mataifa ya kigeni, huku Afrika Kusini – wakati huo ikiwa chini ya utawala wa wazungu wachache – kutuma wanajeshi kuunga mkono Unita, wakati vikosi vya Cuba viliingilia kati upande wa serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!