August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi yaeleza sababu kumkamata kigogo BAVICHA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno

Spread the love

 

JESHI la Polisi nchini Tanzania limetoa sababu ya kumshikilia Mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Twaha Mwaipaya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno, Mwaipaya alikamatwa kwa tuhuma za kuchapisha katika mtandao wake wa twitter habari inazodai zilizua taharuki kwa umma.

Otieno ametoa sababu hizo leo Ijumaa, tarehe 8 Julai, 2022, akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema uchunguzi unaendelea na muda wowote atafikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yake.

“Tunaendelea na uchunguzi na muda wowote tunatarajia kumfikisha Mahakamani kwa kosa la kutoa taarifa za uongo katika ukurasa wake wa Twiter,” amesema Otieno.

Mratibu wa uhamasishaji wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Twaha Mwaipaya

Amesema Mwaipaya alitoa habari hizo za uongo ikiwa yeye sio msemaji wa Serikali wala shirika la umeme nchini Tanzania (TANESCO).

“Serikali ina taratibu zake za kutoa taarifa zake rasmi msemaji wa Serikali yupo na kama ni Tanesco ambao wao wana mamlaka kutoa bei halisi za umeme,” amesema Kamanda Otieno na kuongeza

Itakumbukwa kuwa Mwaipaya alikamatwa tarehe 30, Juni, 2022 na kuachiwa kwa dhamana Jumanne tarehe 5, 2022, baada ya makada wenzake kupaza sauti na kufungua shauri mahakamani kutaka afikishwe mahakamni haraka.

error: Content is protected !!