Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais wa zamani Sudan, al-Bashir kufikishwa ICC
Kimataifa

Rais wa zamani Sudan, al-Bashir kufikishwa ICC

Omar al-Bashir
Spread the love

 

ALIYEKUWA Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, anayesota rumande tangu 2019, kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, yuko mbioni kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kujibu mashtaka yanayomkabili ya mauaji ya kimbali. Inaripoti BBC…(endelea).

Hatua hiyo ni baada ya Baraza la Mawaziri la Mpito la Sudan, kupitisha muswada wa sheria utakaoiwezesha nchi hiyo, kujiunga na ICC.

Taarifa ya Sudan kutaka kujiunga na mhakama hiyo, ilitolewa jana tarehe 3 Agosti 2021 na Waziri Mkuu wa Taifa hilo, Abdalla Hamdok, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hamdok alisema, muswada huo unatarajiwa kupitishwa kuwa sheria hivi karibuni, baada ya mkutano wa pamoja kati ya Baraza Kuu la Uongozi la Sudani na Baraza la Mawaziri la Mpito nchini humo, kuupitisha kuwa sheria.

“Leo (jana), katika mkutano wetu wa Baraza la Mawaziri tumepitisha kwa pamoja muswada wa kujiunga na Mkataba wa Roma wa ICC. Tutafanya mkutano wa mabaraza ya pamoja kuipitisha kuwa sheria. Haki na uwajibikaji ni msingi thabiti wa sheria mpya, sheria ambayo Sudan tunajitahidi kujijenga,” aliandika Hamdok.

Mwezi Februari 2020, Serikali ya mpito ya Sudan ilikubali kumkabidhi Bashir katika mahakama ya ICC, ili ajibu mashtaka ya mauaji ya kimbali na ya kivita, anayodaiwa kuyafanya wakati wa uongozi wake.

Mwanasiasa huyo anatuhumiwa kufanya uhalifu mkubwa wakati wa mzozo wa Darfur, uliotokea 2003 na kusababisha vifo vya watu takribani 300,000.

Licha ya kwamba Sudan haikuwa mwanachama wa ICC, mahakama hiyo ilikuwa inawatafuta washukiwa wa uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari katika eneo la magharibi mwa Darfur.

Akiwemo Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman, maarufu kama Ali Kushayb, ambaye alikuwa kamanda mwandamizi wa kundi la Janjaweed, lililokuwa linaunga mkono Serikali ya Bashir dhidi ya vikundi vya waasi wa Darfur.

Mei 2021, ICC ilihitimisha uthibitisho wa usikilizaji wa mashtaka katika kesi ya Ali Kushayb, anayetuhumiwa kufanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, katika eneo la Darfur kati ya 2003 na 2004.

Bashir aling’olewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi, Agosti 2019 na kupelekea taifa hilo kuunda uongozi wa kiraia, ambao umeapa kutoa haki kwa wahanga wa uhalifu uliofanywa katika Mji wa Darfur nchini humo, wakati wa utawala wake.

Awali, Bashir alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi, akituhumiwa kuwa na utajiri haramu alioupata wakati akiwa madarakani.

1 Comment

  • SHUKURU HUKUUWAWA MPAKA SASA UNAPUMUA DIKTETA AL BASHIR WA SUDAN KILICHO KUKWEKA HAPO GEREANI NI UMWAMBA FAI WA KUJIONA WEWE NDIO KILA KITU WAKATI SI LOLOTE SI CHOCHOTE. UNACHOSTAHIKI WEWE NI KUNYONGWA ILI IWE FUNDISHO KWA MAHARAMIA WENZAKO WANAOWATAWALA RAIA KAMA NG`OMBE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!