June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgeja: Wapotoshaji wa chanjo “ni sawa na magaidi”

Spread the love

 

MWENYEKITI mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja amewafananisha wanaopinga chanjo ya korna (UVIKO-19) na magaidi na kuitaka Serikali iwachukulie hatua. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation amesema hay oleo Jumatano, tarehe 4 Agosti 2021, mara baada ya kupata chanjo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati kuzindua uchanjaji.

“Hawa wanaopotosha kuhusu chanjo ya UVIKO – 19 ni magaidi. Upotoshaji huu ni aina mpya ya ugaidi wachukuliwe kama wahalifu wengine. Kama unazuia watu wasichanjwe maana yake unataka wafe, kwa hiyo hawa ni sawa na magaidi,” amesema Mgeja ambaye mwaka 2015 alihamia Chadema kisha baadaye kurejea CCM

Mgeja amesema, “wanaopotosha dhidi ya chanjo ya UVIKO – 19 wachukuliwe kama wahalifu wengine. Hawa ni sawa na wauaji wa Kimbari. Wachukuliwe hatua za kisheria, tusiwachekee kwani ukicheka na nyani utavuna mabua.”

Amesema taaluma ya kitaalamu inakosolewa kitaalamu siyo kuingiza siasa na upotoshaji hivyo “wanaopinga chanjo ya UVIKO – 19 ni bora wakae kimya au watupe mbadala wa chanjo badala ya kupotosha tu.”

Ametumia fursa hiyo, kump[ongeza Rais Samia Suluhu kwa kukubali Watanzania wapatiwe chanjo na “Mkuu wetu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Sengati kuhamasisha wananchi wapate chanjo, nami nimejitokeza kuwa miongoni mwa Watanzania wa mwanzo kabisa kuchanjwa chanjo dhidi ya UVIKO – 19.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Segati amesema chanjo hiyo inatolewa kwa lengo la mwili kutengeneza kinga dhidi ya janga la corona.

Amesema chanjo dhidi ya UVIKO – 19 ni salama hivyo kuwasihi wananchi walio tayari kuchanjwa wajitokeze kuchanjwa huku akiwataka kuwapuuza wanaopinga chanjo hiyo.

Amesema, kwa awamu ya kwanza wamepokea dozi 25,000 katika mkoa wa Shinyanga ambazo zitatolewa katika vituo 18 katika mkoa.

error: Content is protected !!