Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia amwapisha Silima kuwa Balozi wa Comoro
Habari za Siasa

Rais Samia amwapisha Silima kuwa Balozi wa Comoro

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuapisha Pereira Ame Silima (62) kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Silima ameapishwa leo Jumapili, tarehe 7 Novemba 2021, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma kuchukua nafasi ya Sylvester Mabumba ambaye haijaelezwa amestaafu au atapangiwa majukumu mengine.

Amewahi kuwa Mbunge wa Chumbani visiwani Zanzibar. Aidha, akiwa mbunge alipata fursa kuhudumu nafasi ya naibu waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri wa wizara ya fedha.

Katika uchaguzi mkuu uliopita wa Oktoba 2020, Silima alijitosa kwenye mbio za urais ndani ya chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar kutaka kuchukua nafasi iliyokuwa inaachwa wazi na Dk. Ali Mohamed Shein.

Hata hivyo, mwisho wa kinyyng’anyiro hicho, Dk. Hussein Ali Mwinyi alipitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM kupeperusha bendera ya chama hicho na baadaye kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika 27 na 28 Oktoba 2021, akashinda uchaguzi mkuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!