Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Rais Samia aipongeza Camel Oil kwa mradi wa bilioni Zanzibar
Biashara

Rais Samia aipongeza Camel Oil kwa mradi wa bilioni Zanzibar

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza  Kampuni ya Camel Oil kwa kufadhili ujenzi wa mradi wa kituo cha michezo cha kufurahisha watoto kuanzia miaka mitano hadi 18. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mradi huo unaofadhiliwa na kampuni ya Camel Oil ya Tanzania, utagharimu zaidi ya Sh bilioni moja na itachukua hadi miezi 12 kukamilika.

Rais Samia ametoa pongezi hizo jana Jumatano Kizimkazi Visiwani Zanzibar wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo.

Rais Samia ameupongeza uongozi wa kampuni hiyo na kusema umekuwa mtekelezaji na si watu wa maneno.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Edha Abdallah amesema mradi huo utakapokamilika unatarajiwa kuwanufaisha wakazi wa Kibuteni, Kizimkazi, Kusini Unguja.

Amesema mbali ya eneo la kuchezea pia kutakuwa na kumbi za sherehe na sehemu za kupumzikia watu wazima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!