Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Museveni amlilia Spika wa Bunge
Kimataifa

Rais Museveni amlilia Spika wa Bunge

Spread the love

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni jana tarehe 20 Machi, 2022 ametangaza kifo cha Spika wa Bunge la 11 la Uganda, Jacob Oulanyah. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

 

Oulanyah aliyekuwa akipatiwa matibabu huko Seattle nchini Marekani alikuwa Spika wa Bunge la 11 la Uganda kuanzia 2021 – 2022.

Katika ujumbe wake wa rambirambi, Museveni amesema Oulanyah ni kada mzuri, na kwamba alilazimika kuchelewesha tangazo hilo ili watoto wake wapate taarifa kwanza.

“Nilipata taarifa za habari hizi za kusikitisha saa 10.30 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki kutoka kwa watu ambao wamekuwa naye pamoja na daktari aliyekuwa akimuuguza katika chumba cha wagonjwa mahututi, ” Museveni amesema.

Marehemu Spika alichaguliwa kushika nafasi hiyo Mei 24, 2021, baada ya kumshinda aliyekuwa Spika Rebecca Alitwala Kadaga.

Alikuwa pia Naibu Spika wa Bunge la Uganda, kuanzia Mei 2011 hadi Mei 2021.

Oulanyah pia alikuwa mbunge anayewakilisha Eneobunge la Kaunti ya Omoro, Wilaya ya Omoro, eneo dogo la Acholi, katika Mkoa wa Kaskazini mwa Uganda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!