Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli ashutumiwa na ukabila
Habari za Siasa

Rais Magufuli ashutumiwa na ukabila

Rais John Magufuli akishuka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania
Spread the love

TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema amemvaa tena Rais John Magufuli na sasa amemshutumu kwa kuendesha nchi kwa misingi ya upendeleo wa kikabila na kikanda, anaandika Jovina Patrick.

Lissu amewaambia waandishi wa habari: “Nani anaweza kubisha kwamba Rais Magufuli anaendesha nchi kwa misingi ya upendeleo wa kifamilia, kikabila na kikanda?”

Mwanasheria huyo amesema kitendo cha Rais Magufuli kujenga uwanja wa ndege wilayani Chato ni dhahiri kuwa umejengwa kwa upendeleo kwani hakuna anayejua bajeti yake wala kama ulikidhi vigezo vya kujengwa huko na siyo mikoa mingine.

Lissu amedai kuwa Rais amekuwa akiajiri na kuwapa nyadhifa za juu ndugu zake na watu wanaotoka kanda ya ziwa ili aendelee kuwa na nguvu kubwa ya kuwakandamiza wananchi wa chini.

“Mkuu wa majeshi msukuma, mkuu wa polisi anatoka kanda ya ziwa, mwanasheria mkuu wa serikali anatoka kanda ya ziwa. Anashikilia mpini alafu wananchi wa chini wanashikilia makali na wao ndiyo wanaoumia,” anasema Lissu.

Unaweza kutazama  Video hapo chini kusikia alichozungumza Tundu Lissu

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!