Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vongozi Chadema waachiwa
Habari za Siasa

Vongozi Chadema waachiwa

Spread the love

VICENT Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema, wabunge wawili na viongozi wengine waliokamatwa juzi na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma leo wameachiwa, anaandika Mwandishi wetu.

Taarifa za kuachiwa huru kwa viongozi hao imetolewa na Tumaini Makene, Afisa Habari wa Chama hicho ambapo waliokamatwa ni pamoja na Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na Mbunge wa Viti Maalumu, Zubeda  Sakuru kwa kile kilichoelezwa kuwa ni maagizo aliyopewa ODC wa Nyasa kuwakamata na kuwaweka selo kwa saa 48.

Wengine waliokuwa wamekamatwa ni Philbert Ngatunga (Katibu wa Kanda), Ireneus Ngwatura (M/kiti Mkoa), Delphin Gazia (Katibu Mkoa), Asia Mohamed (Afisa Kanda), Cuthbert Ngwata (M/kiti Wilaya), Charles Makunguru (Mwenezi Wilaya).

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho amesema “Tumepata taarifa viongozi wentu akiwemo Katibu Mkuu wetu na kuwa kesho wanatakiwa kutipoti, sasa haieleweki ni kwa RPC au ni kwa Mkuu wa Mkoa au kwa mkubwa gani mwengine lakini tumeambiwa kuwa anatakiwa kutipoti mahali.

“Hivi tunavyozungumza utaratibu unafanywa kwa taarifa ambazo sina sababu ya kuzitilia shaka Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu kufikishwa Mahakamani na kushitakiwa kwa kosa kwa kosa la uchochezi”.

Lissu amesema, kuna wanachama wa Chadema zaidi ya 51 Wilayani Chato ambao walidiliki kuifanya mkutano wa ndani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!