MTANDAO wa kijamii wa Telegram, umeahidi kuwa utafunga akaunti zinazohusiana na ugaidi nchini Indonesia, anaandika Hamisi Mguta.
Maamuzi hayo ni kufuatia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia nchini humo kufunga huduma za mtandao huo nchini humo siku ya Ijumaa kwa kudai kuwa Telegram imetumiwa kuunga mkono itikadi kali na kutoa maelekezo ya kufanya mashambulizi.
Taarifa kupitia BBC zinaeleza kuwa Pavel Durov, Mwanzilishi wa mtandao huo kupitia taarifa yake amesema kuwa Telegram sasa imeondoa akaunti zote zinazohusika na ugaidi zilizotajwa na serikali.

Hatua hiyo inakuja huku kukiwa na wasiwasi wa kuibuka kwa kundi la Islamic State kusini mashariki mwa Asia ambalo limedai kuhusika kwenye mashambulizi kadhaa nchini Indonesia mwaka huu na limepigana na jeshi mjini Marawi katika kisiwa cha mindanao nchini Ufilipino.
Leave a comment