Friday , 24 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Vifo vitokanavyo na UKIMWI vyapungua
AfyaHabari za Siasa

Vifo vitokanavyo na UKIMWI vyapungua

Spread the love

VIFO vinavyosababishwa na Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI), vimepungua kutoka 29,000 (2022) hadi 22,000 (2024), wakati vitokanavyo na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) vikipungua kutoka 25,800 hadi 18,100. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 13 Mei 2024, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2024/25.

Ametaja takwimu hizo akielezea mafaniko ya utekelezaji bajeti ya mwaka wa fedha unaoisha wa 2023/24.

Pia, Ummy amesema vifo vya wajawazito vimepungua kutoka 556 kwa kila vizazi hai 100,000 (2016) hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000. Kupungua kwa vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kutoka vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 hadi kufikia vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000.

Mafanikio mengine yaliyotajwa na Ummy ni, ongezeko la vituo vya kutolea huduma za afya 1,144, vilivyoongezeka kutoka 8,549 (2021) hadi kufikia 9,693 (2023). Ongezeko la vifaa tiba ikiwemo, MRI kutoka saba hadi 13. CT-Scan (12 hadi 45), Digital X-Ray (147 hadi 346), Ultrasound (476 hadi 668) na Echocardiogram (95 hadi 102).

“Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa ya dharura, zimeongezeka kutoka saba mwaka 2020 hadi kufikia 116 Machi 2024. Huduma za ubingwa na ubingwa bobezi kwa gharama nafuu pia kuvutia wagonjwa kutoka nje ya nchi, ambapo wameongezeka kutoka 5,705 hadi 7,843,” amesema Ummy.

Waziri huyo wa afya ametaja mafanikio mengine kuwa ni, ongezeko la idadi ya vitanda kwa ajili ya wagonjwa mahututi (ICU), kutoka 258 (2021) hadi kufikia 1,362 (2024). Hali ya upatikanaji wa dawa aina 29, katika vituo vya kutolea huduma za afya vya umma imeongezeka kutoka asilimia 58 hadi kufikia asilimia 79 Machi 2024.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka makatibu mahsusi kujiendeleza, kuwa kielelezi cha huduma bora

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia muonee huruma Dk. Phissoo

Spread the loveRAIS wangu mama Samia, wiki iliyopita baada ya kuwa nimekuandikia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 63 ya Uhuru bila katiba ya wananchi

Spread the loveWAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wanaharakati...

AfyaMakala & Uchambuzi

Uongo, uzushi, tiba ya matende, ngiri maji

Spread the loveKUNA uongo na uzushi katika jamii kuhusu wanaume, wanawake na...

error: Content is protected !!