Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Msukuma aibana Serikali ujenzi nyumba za watumishi Geita DC
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Msukuma aibana Serikali ujenzi nyumba za watumishi Geita DC

Joseph Msukuma
Spread the love

MBUNGE wa Geita, Joseph Msukuma (CCM) ameishauri Serikali kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa Halmashauri 31 zilizoanzishwa mwaka 2019 ikiwamo Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Msukuma ametoa kauli hiyo leo Jumatatu bungeni jijini Dodoma baada ya kujibiwa swali la msingi alilohoji ni lini Serikali itawezesha ujenzi wa nyumba za Watumishi wa Geita DC kupitia Watumishi Housing na NHC kisha Halmashauri kulipa kwa awamu.

Akijibu swali hiyo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Zainabu Katimba amesema katika mwaka wa bajeti 2023/2024 Serikali imetenga 37.18 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya ofisi na nyumba za viongozi.

“Kwa hiyo tunatarajia pia halmashauri zitenge bajeti zake kwa mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi nyumba za watumishi, pia ziwe bunifu katika vyanzo vipya vya mapato ili kumudu majukumu yake ikiwemo ujenzi wa nyumba za watumishi. Licha ya kwamba serikali imetenga bajeti naomba nisisitize halmashauri zitenge bajeti kujenga miundombinu muhimu kwa ajili ya watumishi wake,” amesema Katimba.

Amesema serikali itaendelea kuzijengea uwezo mamlaka za serikali za mitaa kuzingatia utaratibu bora wa jinsi ya kutumia fursa zilizopo kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizopo ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

“Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeshapewa utaratibu wa uingiaji wa mikataba na mashirika yanayojihusisha na ujenzi. Halmashauri ya Wilaya ya Geita iandae maombi maalum kwa Watumishi Housing, NHC na TBA ili ijumuishwe kwenye miradi ya ujenzi wa nyumba za Watumishi,” amesema.

Naye Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete naye aliongeza kuwa wizara hiyo kupitia Watumishi housing iinvestiment imeandaa mpango kabambe wa kujenga kwa halmashauri zote.

Amesema kwa kuanza kupitia mpango huo, watajenga nyumba 51, katika halmshauri sita ikiwemo Dodoma.

“Kwa upande wa Geita nitaomba baada ya kikao tukutane na Mhe. Msukuma tutamueleza juu ya mkakati huo ili wao (Geita DC) pia wawe sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!