Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Raia 10,749 wauwa katika vita Ukraine, mazingira yatajwa kuibeba Urusi
Kimataifa

Raia 10,749 wauwa katika vita Ukraine, mazingira yatajwa kuibeba Urusi

Spread the love

 

RAIA wa Ukraine takribani 10,749, wamefariki dunia huku 15,599 wakijeruhiwa katika vita inayoendelea nchini humo. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo kwa msaada wa mashirika ya kimataifa … (endelea).

Taarifa ya vifo hivyo, imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Idara ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Ukraine, Yury Belousov, akihojiwa na Shirika la Interfax la nchini humo, huku akidai idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Akizungumza na shirika hilo, Belousov alidai watu hao wakiwemo watoto 499, wamepoteza maisha tangu vita kati ya Ukraine na Urusi, ianze Februari mwaka jana.

“Tuna uthibitisho wa vifo vya raia 10,749 na majeruhi 15,599, idadi hii inajumuisha watoto 499 waliouawa na watoto 1090 waliojeruhiwa. Hata hivyo, idadi ya vifo inaweza kuongezeka wakati Ukraine itakapotaka kudhibiti maeneo yanayokaliwa na Urusi,” amesema Belousov.

Awali, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN), ilitoa ripoti iliyodai kuwa, watu 9,369 wamepoteza maisha kutokana na vita hiyo.

Hata hivyo, wataalamu wa UN wanadai idadi ya vifo iliyoripotiwa ni ndogo ukilinganisha na hali halisi katika maeneo ya Mariupol, Severodonetsk na Lysychansk, ambako inadaiwa maelfu ya raia waliuawa kutokana na majeshi ya Urusi kulipua mabomu kwenye miji inayokaliwa na raia.

Wakati idadi ya raia wakiendelea kupoteza maisha, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, imedai mazingira ya Ukraine yanaisaidia Urusi kuendelea na mapigano kwa kuwa kuna vichaka vingi vinavyosaidia wanajeshi wake kujificha.

Katika ripoti yake ya ujasusi ya kila mara inayotolewa na wizara hiyo inadai, vichaka hivyo vinasababishwa na mashamba yaliyotelekezwa kusini mwa nchini Ukraine, tangu vita ianze.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!