Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Puma Tz yakabidhi vifaa tiba vya mil. 6.5 Kogamboni
Habari Mchanganyiko

Puma Tz yakabidhi vifaa tiba vya mil. 6.5 Kogamboni

Spread the love

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imekabidhi msaada wa vifaa tiba vikiwemo vya viti mwendo na mashine za kupima presha vyenye thamani ya Sh.milioni 6.5 ambavyo vitatumika katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Fatma Abdallah amesema katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, kampuni hiyo imeona ina kila sababu ya kuwagusa wanawake kupitia vifaa tiba hivyo ambavyo wamekabidhi.

“Puma tumekuja kukabidhii vifaa tiba katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, tumejitahidi kukusanya vifaa tiba kadhaa vyenye thamani ya Sh.milioni 6.5. Tunavyo vifaa tiba vya kila kama viti mwendo na mashine za kupima presha , tunaamini vitasaidia wodi ya wanawake.Tunafamu wodi ya akina mama ni eneo lenye changamoto nyingi na wagonjwa wengi.

“Hivyo inahitaji uangalizi tofauti , sio kwamba tunajipendelea sisi wanawake lakini wodi ya wanawake inahitaji uangalizi wa tofauti kidogo,”amesema Fatma Abdallah huku akielezea kuwa katika kampuni yao wameendelea kuongeza idadi ya wafanyakazi wanawake.

Amefafanua Puma kuna wanawake zaidi ya 48 na hatua kubwa imepigwa kaunzia mwaka 2023 kwani wakati anaingia Puma mwaka jana kulikuwa na wafanyakazi wanawake asilimia 9 lakini sasa hivi imefika asilimia 16 huku akisisitiza wanawake wengi wameingizwa kwenye uongozi.

Hata hivyo, amesema wanaendelea kutengeneza mazingira kuwawezesha, kuwathaminisha na kuwaleta pamoja wanawaje ili waweze kuleta maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

“Puma tutaendelea kusaidia sekta ya afya kama tulivyosema, tunaangalia sekta ya afya na sekta ya elimu,”amesema huku akikumbusha kuhusu Puma ni kwamba ni kampuni kubwa inayojuhusisha na sekta ya mafuta ni kampuni ambayo inawabia wawili.


“Sisi tunaongoza katika soko la mafuta lakini bado tunaendelea kukua , tunaimani maono yetu ni kuhakikisha tunafikia wananchi wengi ambao hawapati huduma ya mafuta kwa ukaribu.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi, Matroni Eva Sambaya amesema wanashukuru kupatiwa vifaa hivyo na Puma imeonesha kuwathamini na kuwajali kwani ziko hospitali nyingi katika jiji la Dar es Salaam.

“Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani Puma mmeona haja ya kuja kwetu na kutushika mkono , vifaa hivi kwetu vitasaidia katika kutoa huduma katika wodi ya wanawake.”

Wakati huo huo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni(DMO) Dk.Lucas Ngamtwa amesema wanatoa shukrani za dhati kwa kampuni ya Puma kwa namna ambavyo wameguswa na kuamua kuwashika mkono katika hospitali hiyo.

“Hospitali yetu ni mpya bado tunachangamoto nyingi ikiwemo ya watalaam na vifaa tiba lakini kwa kutambua hilo Kampuni ya Puma mmeona mje mtushike mkono kwa kuhakikisha akina mama wanaokuja kupata huduma katika hospitali yetu wanakuwa salama na wanajifungua katika mazingira mazuri,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!