Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Uchaguzi 2024/2025 kufa kupona, atakayeshindwa kuusimamia ang’oke
Habari za Siasa

Mbowe: Uchaguzi 2024/2025 kufa kupona, atakayeshindwa kuusimamia ang’oke

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa(CHADEMA), Freeman Mbowe ameagiza uongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya taifa hadi shina kupitia mabaraza yote  kuhakikisha wanasimamisha mgombea katika nafasi yoyote inayotakiwa kugombewa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (Endelea).

Ametoa maagizo hayo leo tarehe 8 Muchi 2024 wakati wa hotuba ya siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa Kitaifa na Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) katika ukumbi wa CBC Jijini Dodoma.

Katika maagizo yake Mbowe kwa wanachama wa chama hicho amesema kiongozi yoyote ambaye atashindwa kusimania mchakato wa kuwapata wagombea katika nafasi zote kwa ngazi ya Serikali za Mitaa na kuelekea uchaguzi mkuu 2025 ni bora ajiondoe mapema katika uongozi katika nafisi hiyo.

Aidha, amewaagiza viongozi wote ndani ya chama  kuhakikisha wanaweka wagombea ambao nia yao ni ushindi na siyo kwa ajili ya kujaza nafasi.

Katika hatua nyingine Mbowe amesema akina mama wa Chadema wanatakiwa kuendeleza nguvu zao kubwa kuhakikisha wanapiga kelele kwa ajili ya kudai katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi.

Pia amewahamasisha kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu ni uchaguzi wa kufa na kupana hivyo hakuna muda wa kusubiri ushindi wa muujiza.

Hata hivyo, ameeleza kuwa Chadema ni kati ya chama ambacho kwa sasa kinatazamwa na watu wengi kwa maana ya kutetea haki za watu kwa maana wameishakata tamaa ya maisha kutokana na maisha kuwa magumu na kutozingatia haki na demokrasia.

Amesema kila mwanachama ndani ya chama anatakiwa kuwa muumini wa kudai haki na kuheshimu misingi ya demokrasia kwa kuhamini kuwa haki na demokrasia ndiyo msingi wa uongozi ulio mwema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika amesema chama bado kinaendelea kupambana kwa lengo la kupata katiba mpya pamoja na upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi isiyokuwa na matatizo.

Amesema kuwa pamoja na serikali kueleza kuwa inafanya marekebisho lakini bado kuna ujanja ujanja kwani mpaka sasa wakurugenzi wanaweza kuendelea kusimamia uchaguzi kwa mujibu wa katiba ilivyo sasa.

Kwa upande wake Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khanani amesema kuwa wakati Bunge linapitisha miswada ya marekebisho ya Katiba mpya na tume ya uchaguzi serikali halikuzingatia maoni ya wadau hivyo maoni mengi yaliachwa.

Amesema maoni mengi ya wabunge hupitishwa kwa kura hivyo wabunge waliowengi ambao ni wa CCM kura zao zilipitishwa miswada hiyo mibovu.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Bawacha Catherine Rugge amesema serikali inaendelea kujinufaisha na kujipendelea kwa kuongezea mafao viongozi wastaafu pamoja na wake zao wakati watanzania wanaendelea kuumia na maisha magumu.

Amesema kuwa ni busara kurekebisha sheria ya jinsi ya kuwalipa viongozi wastaafu na wenza wao ili kuboresha maisha ya watu wengine wa hali ya chini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!