Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Profesa Kitila aahidi neema wenye viwanda Tanzania
Habari za Siasa

Profesa Kitila aahidi neema wenye viwanda Tanzania

Spread the love

 

WAZIRI wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Profesa Kitila Mkumbo amesema, Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto kwenye bidhaa za ndani hususan kodi na masoko ili kuvipa nguvu viwanda viweze kukua zaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Profesa Kitila alisema hayo jana Jumamosi, tarehe 16 Oktoba 2021, wakati alipotembelea viwanda vya uzalishaji wa transfoma, nyaya na vifaa vya umeme vinavyomilikiwa na kampuni ya Kilimanjaro Cables (AFRICABLE).

Amewaomba Watanzania kuona haja ya kutumia vifaa vinavyozashwa nchini humo ili kuvifanya kukua zaidi kwani haoni haja ya kuagiza vifaa vya umeme kutoka nje ya nchi kwa kuwa kwa sasa viwanda vya ndani vina uwezo wa kuzalisha vifaa hivyo vinavyotosheleza mahitaji na vingine kuuzwa nje ya nchi zikiwemo transfoma.

Profesa Kitila alisema, nia ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona viwanda vya ndani vinazidi kuwa vyenye nguvu na ubora katika uzalishaji ili kuleta ushindani na viwanda vya nje jambo ambalo pamoja na mambo mengine litasaidia kulitangaza taifa.

“Nimetembelea viwanda hivi na kujionea hali halisi ilivyo hasa kuhusu uzalishaji, natambua changamoto zilizopo kwenye bidhaa za ndani ikiwemo suala la kodi na masoko, Serikali inakwenda kutatua haya yote kwa lengo la kuvipa nguvu zaidi viwanda vyetu vya hapa nchini,” alisema Profesa Mkumbo .

Alisema uwekezaji wa kiwanda hicho, mbali na kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama, pia umesaidia kuharakishwa kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme nchini ikiwemo ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA) hatua inayoendelea kuliletea maendeleo Taifa na hivyo kusisitiza haja ya wawekezaji hao kuendelea kuthaminiwa.

Waziri huyo alisema kwa kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa mwekezaji huyo na mkakati wake wa ujenzi wa mtaa maalumu wa uwekezaji wa viwanda vyake vyote katika eneo moja huko Kimbiji Kigamboni, wataboresha miundombinu katika wilaya ya kigamboni ili kurahisisha mazingira yote ya kufika eneo hilo.

Awali, Meneja Masoko wa kiwanda hicho, David Tarimo alisema wataendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora na zinazokidhi mahitaji ya Watanzania ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuwa na viwanda bora kwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Alisema wao kama wawekezaji wazalendo wa hapa nchini, jukumu lao ni kuhakikisha wanaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha sekta ya nishati nchini inakuwa yenye tija kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora zitakawawezesha wananchi kuzitumia kwa muda mrefu.

Tarimo alisema changamoto wanayokabiliana nayo ni baadhi ya wananchi kuendelea kuamini bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi ambazo nyingi zimekuwa zikiingizwa kwa njia ya panya na zaidi zikikosa ubora ikilinganishwa na bidhaa zinazozalishwa nchini ,

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Wanaotaka kujifunza ZEC kwao kukoje?

Spread the loveMKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Biteko, Nape wanadanganya?

Spread the loveKWA mila na desturi zetu za Kiafrika mkubwa huwa hakosei,...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miamka 60 ya Muungano: Tunakwama wapi?

Spread the loveRAIS wa Jamhuri, Samia Suluhu Hasssan, Ijumaa iliyopita, aliongoza mamilioni...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

error: Content is protected !!