Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki
Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the love

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza Kardinali wa Marekani, Raymond Burke anayedaiwa kuwa mkosoaji mkubwa na mpingaji wa mpango wake wa kufanya mageuzi ndani ya kanisa hilo. Inaripoti BBC Swahili…(endelea).

Mtandao huo umeripoti kuwa, Papa Francis alitangaza uamuzi wa kuchukua hatua dhidi ya Kardinali Burke, katika mkutano wake na wakuu wa ofisi za Vatican, uliofanyika wiki iliyopita.

Papa Francis

Hadi sasa imeripotiwa kuwa, Papa Francis ana mpango wa kumfukuza Kardinali Burke katika makazi yake kwenye makao makuu ya kanisa hilo, Vatican, pamoja na kusitisha mshahara wake.

Inadaiwa kuwa, Kardinali Burke ni sehemu ya kundi la mapadri wa Marekani, ambao kwa muda mrefu wamepinga mipango ya Papa Francis kuleta mageuzi katika Kanisa Katoliki.

Taarifa ya Kardinali Burke kufukuzwa, zimekuja takribani mwezi mmoja tangu Papa Francis amfukuze kazi, Joseph Strickland, aliyekuwa kiongozi wa kanisa hilo katika jimbo la Texas, anayedaiwa kuhamisha kanisa kwenye msimamo wa kiliberali kuhusu utoaji mimba, haki za watu waliobadili jinsia na ndoa za jinsia moja.

Mwandishi wa BBC, Christopher White, amedai kuwa, uamuzi huo unaweza kuchochea upinzani mkubwa na kuongeza mgawanyiko kati ya Vatican na kanisa la Marekani.

Kardinali Burke aliyeteuliwa na mtangulizi wa Papa Francis, Papa Benedict XVI, anadaiwa kuwa kwenye mvutano mkali na kiongozi huyo kwa muongo mmoja, ambapo anamkosoa kuhusu masuala ya kijamii na liturjia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!