Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bihimba awakumbuka watoto yatima Msongola
Habari Mchanganyiko

Bihimba awakumbuka watoto yatima Msongola

Spread the love

MWANAHARAKATI huru, Bihimba Mpaya ametoa msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula, katika Kituo cha Watoto Yatima Msongola, kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam, huku akiahidi kuwanunulia vifaa vya shule kila mmoja, ifikapo mwanzoni mwa 2024. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Bihimba ametoa msaada huo leo tarehe 30 Novemba 2023, jijini Dar es Salaam, baada ya mlezi wake, Christina Haule, kumuomba msaada.

“Mama yangu alinipigia simu akaniambia kuna changamoto ya chakula kwenye kituo chetu, nikamwambia nitakuja leo, nashukuru Mungu nimeweza kufika. Nimewaletea chakula, mchele kilo 50, unga, mafuta ya kula, sukari, maharage na vitu vingine,” amesema Bihimba na kuongeza:

“Nadhani ndugu zangu tutaendelea kushirikiana na watoto hapa wengi ni wanafunzi, shule zikifunguliwa nitawapatia sare mpya za shule wote pamoja na vifaa vingine. Nafanya hivi kwa sababu nataka watoto wapate elimu.”

Kwa upande wake Haule, amesema kituo hiko kinakabiliwa na changamoto mbalimbali, hususan chakula na mahitaji mengine, ambapo amewaomba wadau wengine wajitokeze kutoa msaada.

Bihimba Mpaya

Aidha, Haule amemshukuru Bihimba kwa kutoa msaada huo, huku akisema utawasaidia watoto yatima 86 wanaolelewa katika kituo hicho kilichoanzishwa 2006.

Watoto hao kupitia kwa wawakilishi wao, Glory Stanslaus na Ramadhan Suleiman, wamemshukuru Bihimba kwa kuwapa msaada wa chakula, huku wakimuombea Baraka kwa Mwenyezi Mungu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!