BENKI ya NMB nchini Tanzania imetoa msaada wa viti 15, meza 10, kabati moja pamoja na viti vya wageni viwili kwa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Msaada huo uliokabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya NMB, Martine Massawe kwa Mwenyekiti SHIUMA, Ernest Masanja ni maalum kwa ajili ya ofisi ndogo ya makao makuu ya shirikisho hilo jijini Dar es Salaam.
Katika makabidhiano hayo pia alikuwepo, Makamu Mwenyekiti wa SHIUMA, Taifa, Stephen Lusinde na Mkurugenzi anayeratibu Makundi Maalum (Machinga) kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Juma Samwel.
Leave a comment