Wednesday , 22 May 2024
Home Gazeti Tangulizi Rais Samia: Kaya zote hazitofikiwa siku ya sensa
Tangulizi

Rais Samia: Kaya zote hazitofikiwa siku ya sensa

Kamishna wa Sensa na Makazi ya Watu Tanzania, Anna Makinda
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi ambao hawatafikiwa kesho tarehe 23 Agosti, 2022 na makarani wa sensa kuhakikisha wanatunza kumbukumbu za watu wote waliolala katika kaya zao usiku wa Agosti 23 mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema makarani hao hawataweza kufikia kaya zote kwa wakati mmoja kesho kutokana na ukubwa wa nchi.

Akihutubia wananchi leo usiku tarehe 22 Agosti, 2022 Rais Samia amesema taarifa zitakazoachwa na wakuu wa kaya zitamsaidia karani atakapopita azikute na kuziingiza kwenye mfumo wa kukusanyia taarifa.

“Kama kutahitajika ufafanuzi wowote muwe tayari popote mlipo kutoa ushirikianio wa kutosha hata kwa njia ya simu,” amesema Rais Samia.

Amesema wakuu wote wa kaya nchini watapewa fomu maalumu ambayo watajaza majina matatu ya wanakaya wao, jina lake, jina la baba, babu, umri, wake, jinsia, simu za kiganjani na taarifa nyingine muhimu zilizopo kwenye dodopso la sensa.

Rais Samia Suluhu Hassan

“Kwa mnasaba huo niwasihi kila mmoja wetu siku hiyo kuacha namba za simu nyumbani au kwa kiongozi wa kitongoji, mtaa au shehia yake ili aweze kupatikana na karani wa sensa ikiwa kutajhitajika taarifa za ziada. Baada ya tarehe 23 zoezi bado litaendelea kukamilishwa wakati wananchi tukiendelea na shughuli zetu za kawaida,” amesema.

Amesema siku ya sensa ya watu na makazi, ni maalumu ambayo hutokea kila mara moja baada ya miaka 10.

“Tanzania wakati huo, sensa ya mara ya kwanza ilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012. Na hata kabla ya uhuru kumbukumbu zinaonesha Tanzania Bara au Tanganyika ilifanya sensa tano, ya kwanza ilifanyika 1913, 1921, 1931, 1948 na 1957 ilihali Zanzibar ilifanywa mara moja 1958 wakati wa ukoloni wa Sultan.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

KimataifaTangulizi

Rais Iran afariki kwa ajali ya helkopta

Spread the loveRais wa Iran, Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!