Tuesday , 21 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia: Kosa la jinai karani kutoa taarifa za kaya
Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kosa la jinai karani kutoa taarifa za kaya

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema taarifa zitakazokusanywa na makarani wa sensa nchi nzima ni taarifa za siri kwa mujibu wa sheria ya takwimu sura 321.

Amesema karani wa sensa haruhusiwi kutoa siri ya taarifa alizokusanya katika kaya akifanya hivyo kwa makusudi ni kosa la jinai hivyo hatua za kisheria zinatachukua mkondo wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akihutubia wananchi leo usiku tarehe 22 Agosti, 2022 amesema kukamilika kwa sensa ya watu na makazi mwaka huu ndio dira kwa maendeleo ya nchi kwa miaka ijayo.

Amesema sensa ya mwaka 2022 ni ya sita kufanyika tangu kuasisi kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1964, hivyo kwa mamlaka aliyopewa na kwa mujibu wa sheria ya takwimu ya sura 351, (6)(2)(a) na (21), anawakumbusnba wananchi wote kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kesho tarehe 23 Agosti, 2022.

“Naomba kila mmoja wetu ahakikishe anakuwepo wakati wa kuhesabiwa na kujibu kwa ufasaha maswali yote yatakayoulizwa na makarani wa sensa watakaotutembelea katika kaya zetu.

“Itakumbukwa sensa zote zilizolipita zilikuwa zinafanyika siku ya Jumapili ya mwisho wa mwezi wa Agosti lakini imebainika kuwa hii inaingilia na siku ya ibada ambapo baadhi ya waumini huwa hawapo majumbani wakati makarani wa sensa wanapopita. Kwa kuzingatia hilo serikali imeamua tarehe 23 Agosti iwe siku ya mapumziko,” amesema.

Amesema makarani wa sensa waliwasili tarehe 21 katika eneo waliyopangiwa nchi nzima ikiwa ni siku mbili kabla ya zoezi kuanza nchi nzima.

“Lengo ni kujitambulisha rasmi kwa viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na shehia, kutambua mipaka ya eneo la kuhesabia watu walilopangiwa, kukusanya taarifa muhimu na kuandaa ratiba inayoonesha muda na siku za kutembelea kaya zote zilizopo katika eneo husika siku ya tarehe 23. Utaratibu huu ni kurahisisha na kulifanya zoezi liwe kwa urahisi,” amesema.

Amesema umuhimu wa sensa umeshaelezwa kuwa kwanza kupata taarifa kamili ambazo zitaisaidia serikali kuandaa vizuri zaidi mipango ya maendeleo.

Pia baadhi ya majibu yatapima na kutathmini utekelezaji wa ajenda za kikanda na kimataifa kama vile dira ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2050, ajenda ya maendeleo ya Afrika ya 2063, ajenda ya maendeleo endelevu ya dunia ya 2030.

“Aidha, sensa ya mwaka huu ina umuhimu wa kipekee kwa vile imeunganisha sensa ya majengo yote nchi nzima kwa ajili ya kufahamu kiwango cha ubora wa makazi ya wananchi wanayoishi.

“Jambo ambalo halijawahi kufanyika hapa nchini, kukamilika kwa zoezi hili kutaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kuunganisha sensa ya watu na makazi,” amesema Rais Samia.

Amesema matokeo ya mwanzo ya sense hiyo yatatoka mapema mwezi Oktoba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

error: Content is protected !!