Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Nchimbi: Uhusiano wa Tz, Urusi kuboreshwa kunufaisha pande zote
Habari Mchanganyiko

Nchimbi: Uhusiano wa Tz, Urusi kuboreshwa kunufaisha pande zote

Spread the love

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema CCM chini ya Mwenyekiti Rais Samia Suluhu Hassan, itaendelea kudumisha uhusiano na urafiki wa muda mrefu kati ya Tanzania na Urusi, ukilenga kuboresha maeneo ya uwekezaji, biashara na uchumi, kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan, ambapo amesisitiza kuwa kuboresha maeneo ya uwekezaji, biashara na uchumi, kutaimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali za nchi hizo mbili na wananchi wake na kuufanya kuwa wa moja kwa moja zaidi.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Alhamis, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, pamoja na kurejea kumbukumbu za uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Urusi.

Amesema tangu wakati wa kupigania uhuru na baada ya uhuru, ambao mwaka huu unafikisha miaka 62, walizungumzia maeneo ambayo yanaweza kufanyiwa kazi na Serikali za nchi hizo, chini ya uongozi wa vyama vinavyoongoza nchi hizo, CCM na United Russia, mtawalia.

Kwa upande wake, Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan, mbali ya kumpongeza na kumtakia kila la heri Balozi Dk. Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Ameelezea uhusiano wa muda mrefu wa Urusi kwa Tanzania na nchi za Afrika, tangu wakati wa kupigania uhuru na baada ya uhuru, ambapo ilikuwa mojawapo ya nchi za mwanzo kuitambua Tanganyika huru, akisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais Vladimir Putin, na mazingira mazuri ya uwekezaji, biashara na uchumi ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Urusi iko tayari kuendelea kuenzi na kuimarisha uhusiano utakaonufaisha pande zote mbili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!