Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Nchi 93 zaing’oa Urusi UN, Tanzania yajiweka kando
Kimataifa

Nchi 93 zaing’oa Urusi UN, Tanzania yajiweka kando

Spread the love

JUMLA ya nchi 93 zimepiga kura kuunga mkono pendekezo la kusimamisha uanachama wa Urusi katika Baraza la haki za Binadamu la Umnoja wa Mataifa (UN). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Aidha, katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA), jumla ya nchi 24 zimepiga kura ya kupinga pendekezo hilo huku nchi 58 hazikuwepo katika tukio hilo.

Tanzania na Kenya zilikuwa mojawapo ya nchi ambazo hazikupiga kura juzi tarehe 7 Aprili, 2022 katika baraza hilo huku Burundi ambayo pia ni mojawapo ya nchi za Afrika Mashariki ikipiga kura Urusi kuiondolewa katika Baraza hilo la Haki za Binadamu.

Kutokana na hatua hiyo, Urusi imesimamishwa uanachama kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja huo huku Rais wa Marekani, Joe Biden akitaja ukatili unaoendelea nchini Ukraine kuwa ni ghadhabu dhidi ya ubinadamu.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kundi la mataifa saba tajiri zaidi ulimwenguni (G7), Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani wakizidisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi na hasa kufuatia picha za kutisha zilizosambaa hivi karibuni za miili ya watu wanaodaiwa kuuawa na wanajeshi wa Urusi katika mji wa Bucha na Mariupol nchini Ukraine.

Rais Biden amesema visa vya watu kubakwa, kuteswa na kuuawa na katika baadhi ya matukio mengine miili yao kukatwakatwa ni ghadhabu dhidi ya ubinadamu wao.

Shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa pia linasema ubakaji umekuwa ukitumika kama ngao ya vita nchini Ukraine.

Ukraine na washirika wake wa Magharibi wanavishutumu vikosi vya Urusi kwa kufanya uhalifu wa kivita kwa kuwalenga kwa makusudi raia nchini Ukraine.

Hata hivyo, Urusi imekana madai hayo pamoja na kupinga hatua ya kusimamishwa, kufuatia kura iliyopigwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA), ambayo imeiita kuwa kura isiyo ya haki na iliyochochewa kisiasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!