Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Naibu Waziri amuweka mtegoni Mkuu chuo cha hali ya hewa
Habari Mchanganyiko

Naibu Waziri amuweka mtegoni Mkuu chuo cha hali ya hewa

Spread the love

NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete amemtaka Mkuu wa Chuo cha Hali ya Hewa Tanzania, Peter Mlonganile kuhakikisha anabuni mbinu zaidi za kukitangaza chuo hicho ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ili kitambulike zaidi na hatimaye kuzalisha wataalam wengi zaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza jana tarehe 20 Agosti, 2022 mjini Kigoma baada ya kutembelea Chuo hicho Naibu Waziri huyo amesema wahitimu wa kozi zinazotolewa chuoni hapo ni wa muhimu kwani kila sekta inahitaji wataalam wa hali ya hewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na ushauri kwenye maendeleo mbali mbali ya taasisi za Serikali na binafsi nchini.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Hali ya Hewa, Peter Mlonganile kuhusu maboresho yaliyofanyika katika maabara ya Kompyuta, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Chuo hicho Mkoani Kigoma.

“Kozi zinazotolewa hapa ni muhimu sana na zinahitajika kila sehemu lakini taasisi na wananchi bado hawajafahamu uwepo chuo hiki hivyo Mkuu wa Chuo kuwa mbunifu tangaza chuo hiki ili wanafunzi waje wapate elimu na ujuzi’ amesisitiza Naibu Waziri Mwakibete.

Naibu Waziri Mwakibete amempongeza Mkuu wa chuo kwa kuzingatia thamani ya fedha kwenye usimamizi wa mradi wa maboresho ya majengo mbalimbali chuoni hapo ambao umegharimu takribani milioni 400 na kukamilika kwa wakati na viwango.

Naye Mbunge wa Kigoma Mjini Ng’enda ameishukuru Serikali na kusema kuwa maboresho yaliyofanyika yamekifanya chuo kurejea kwenye hadhi yake kwani kabla ya maboresho wakufunzi walilazimika kutumia mabweni kama ofisi hali iliyokuwa ikishusha hadhi ya chuo hasa ikizingatiwa kinadahili wanafunzi wa ndani na nje ya nchi.

Mbunge Ng’enda ameongeza kuwa maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika yatakuwa fursa kwa wananchi wa Kigoma kwani yatasababisha kuongezeka kwa kipato cha wananchi hao kwani wananfunzi wanahitaji malazi, vyakula na mahitaji mbalimbali wakiwa masomoni.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Peter Mlonganile amesema kwa sasa chuo kinatoa kozi chahce ambapo mipango ya mbeleni ni  kuendeleza mazungumzo na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Fizikia ili kuona namna vyuo hivyo vitakavyoshirikiana kwenye utoaji wa kozi zaidi.

Chuo cha Hali ya Hewa kinamilikiwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambapo kwa sasa kinatoa kozi za ngazi ya Astashahada ya awali, Astashahada na Stashada za masuala ya hali ya hewa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!