Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Yonazi asisitiza ushirikiano sekta binafsi, umma
Habari Mchanganyiko

Dk. Yonazi asisitiza ushirikiano sekta binafsi, umma

Spread the love

WATENDAJI wa taasisi za umma na binafsi ambao wanatekeleza ajenda ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kidijiti wametakiwa kushirikiana na kutekeleza jukumu hilo kwa weledi na ubora wa viwango vya kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Akizungumza katika Jukwaa la Nne la Ubunifu na Teknolojia lililofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 19 Agosti, 2022, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jim Yonazi amesititiza ushirikishaji baina ya sekta ya umma na binafsi ili kutimiza malengo ya kuwa na Tanzania ya Kidijiti tunayoihitaji kwa maendeleo ya Taifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Jim Yonazi (Kulia) akifatilia majadiliano ya Jukwaa la Nne la Ubunifu na Teknolojia yaliyokuwa na Kauli Mbiu ya Tanzania ya Kidijitali Tunayoihitaji, Hatua Zipi Zichukuliwe Kuifikia? lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na kufanyika tarehe 19 Agosti, 2022 jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, kuna fursa nyingi za kiuchumi katika ulimwengu wa kidijiti na Wizara hiyo ipo tayari kupokea na kufanyia kazi maoni ya wadau wa sekta ya umma na binafsi kuhusu nini kinahitaji maboresho katika kufikia dira na malengo ya Taifa ya kuijenga Tanzania ya Kidijiti.

Dk. Yonazi amezungumzia juhudi kubwa inayofanywa na Serikali ya kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inayoendesha uchumi wa kidijiti kwa kuongeza wigo wa usambazaji wa miundombinu na ufikishaji wa huduma za TEHAMA nchini.

“Kama mnavyofahamu hivi karibuni kupitia Shirika letu la Mawasiliano la TTCL tumefikisha intaneti yenye kasi katika Mlima Kilimanjaro na mradi wa kufikisha intaneti majumbani “fiber to home” tayari umeanza kutekelezwa na TTCL lengo ni kufikia uchumi wa kisasa wa kidijiti katika nchi yetu”, amesema Dk. Yonazi

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), Dk. Amos Nungu amesema kuwa Jukwaa la Ubunifu na Teknolojia limewakutanisha wataalamu wabobezi, watafiti, wabunifu na watunga sera ili kujadili na kutoka na taswira tofauti ya kuijenga Tanzania ya Kidijiti kwa kuangazia vipaumbele  na mahitaji ya watanzania.

Jukwaa hilo la Nne la Ubunifu na Teknolojia lilikuwa na kauli mbiu ya Tanzania ya Kidijitali Tunayoihitaji, Hatua zipi zichukuliwe Kuifikia? liliandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kupitia programu ya ubunifu ya FUNGUO na kuwakutanisha wadau wa Sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoka taasisi za umma na binafsi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!