Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwili wa Rais mstaafu Angola kuchunguzwa
Kimataifa

Mwili wa Rais mstaafu Angola kuchunguzwa

Spread the love

MAHAKAMA moja nchini Uhispania, imeruhusu kufanyika kwa uchunguzi wa maiti ya aliyekuwa Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, aliyeaga dunia akiwa mjini Barcelona tarehe 8 Julai, 2022. Inaripoti mitandao ya kimataifa… (endelea).

Binti yake, Tchize dos Santos, aliomba uchunguzi wa maiti yake ufanyike kwa sababu anaamini kulikuwa na mazingira ya kutiliwa shaka kuhusiana na kifo chake.

Alisema mahasimu wake wa kisiasa hawakutaka aunge mkono upinzani, katika uchaguzi ujao wa Angola.

Aidha, mashirika ya habari yameripoti kuwa  mwanasiasa huyo alitaka kuzikwa kwa faragha nchini Uhispania, lakini serikali ya Angola inafanya mipango, ikitaka mwili wake urejeshwe nchini mwake kwa mazishi rasmi ya kiserikali.

Mwanasaiasa huyo mkongwe, aliyekuwa na umri wa miaka 79 alifariki katika zahanati ya Teknon mjini Barcelona, ambako alikuwa akipokea matibabu, na alikuwa ameugua kwa muda mrefu, kulingana na taarifa ya afisi ya rais.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!