Thursday , 2 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwanamke ajifungua watoto saba, madaktari wapigwa butwaa
Kimataifa

Mwanamke ajifungua watoto saba, madaktari wapigwa butwaa

Spread the love

 

NI MIUJIZA! Ndivyo unavyoweza kueleza tukio la Mwanamke mmoja aliyejifungua watoto saba kwa mpigo mjini Abbottabad huko nchini Pakistan. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tukio hilo limetokea juzi tarehe 17 Oktoba, 2021 katika mji wa Abbottabad nchini Pakistan baada ya mwanamke huyo aliyedhaniwa kuwa na ujaunzito wa watoto watano, kujifungua watoto saba.

Akizungumza na waandishi wa habari, mume wa mwanamke huyo, Yar Mohammad amesema Mungu amewajaalia watoto wanne wa kiume na watatu wa kike.

Amesema mkewe aliyejifungua katika Hospitali ya Kimataifa ya Jinnah, hali yake na watoto imeimarika na wanaendelea vizuri.

Mohammed amesema uchunguzi wa awali ulipobaini mke wake amebeba watoto kadhaa tumboni walishauriwa waende hospitali kubwa kwa uangaalizi wa karibu.

Ameongeza madaktari waliomhudumia walishangazwa sana hali ya mkewe.

Aidha, Mmoja wa madaktari bingwa walioongoza jopo la kumfanyia operesheni mwanamke huyo, Dk Hina Fayaz ambaye ni daktari bingwa wa wanawake katika Hospitali hiyo ya Jinnah, amesema mwanamke huyo alifika hospitalini hapo kwa mara ya kwanza Jumamosi tarehe 16 Oktoba mwaka huu.

“Baada ya uchunguzi wa ultrasound na ripoti zingine, tuligundua kuwa ana watoto watano ndani ya tumbo lake na ujauzito wake ulikua wa zaidi ya miezi minane.

“Tulishtuka sana kuona ripoti ya matibabu ya mwanamke huyu.

“Alikuwa na shinikizo la damu iliyotajwa kuwa ya kiwango hatari. Tumbo lake lilikuwa limevimba. Katika uzao wake wa kwanza na wa pili, alikuwa amejifungua watoto wawili kwa njia ya upasuaji, hivyo alikuwa na maumivu makali kwenye kovu la upasuaji wa kwanza,” amesema.

Amesema ni maajabu kuona mama huyo na watoto wake wote wametoka salama.

Aidha, kwa kuwa imelazimu mama huyo kufanyiwa upasuaji na kutolewa watoto hao waliokuwa na umri wa miezi nane kwa maana ya njiti, imebidi wawekwe kwenye chumba maalumu cha uangalizi kwa siku kadhaa kabla ya kuruhusiwa kutoka hospitali.

Hata hivyo, akizungumzia sababu za mwanamke kubeba ujauzito wa mapacha wengi kiasi hicho, Dk. Fayaz amesema sababu kubwa ni matumizi ya dawa za kuchagiza upatikanaji wa ujauzito kupita kiasi.

“Ndio maana huwa tunashauri matumizi ya dawa hizi yatolewe na daktari mwenye ujuzi wa kutosha ili kuokoa maisha ya mama anayehitaji mtoto,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

China inatathmini upya sera za wafanyakazi

Spread the love  WAKATI idadi ya watu wa nchi China inapungua, Beijing...

Kimataifa

Vita vya Ukraine: Boris Johnson adai kutishiwa kupigwa kombora na Putin

Spread the loveALIYEKUWA Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amesema, Rais wa...

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

error: Content is protected !!