Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mtuhumiwa wa utapeli, kudhulumu viwanja aburuzwa mahakamani
Habari MchanganyikoTangulizi

Mtuhumiwa wa utapeli, kudhulumu viwanja aburuzwa mahakamani

Spread the love

Mtuhumiwa wa kutapeli na kudhulumu viwanja vya watu na kujimilikisha kinyume na utaratibu jijini Dar es salaam ajulikanae kama Paul Mushi leo Ijumaa ametolewa kituo cha Polisi Oysterbay na kupelekwa mahakama ya mwanzo Kinondoni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa hapo awali kwa tuhuma za kunyang’anya viwanja vya watu kadhaa na sasa amepekwa mahakamani ili hatua za kisheria ziendelee.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa

Aidha, mapema jana Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa alitangaza kuanza kwa operesheni maalumu ya kudhibiti matapeli wa ardhi katika jiji la Dar es salaam.

Operesheni hii imekuja siku chache tangu kufanyika kwa Kliniki ya Ardhi ya Jijini Dar es salaam iliyoanza mapema mwezi Novemba 2023 na kuhitimishwa tarehe 3 Machi 2024 kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi iliyokuwa inasumbua jiji la Dar es salaam kwa muda mrefu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

error: Content is protected !!