Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT -Wazalendo watishia kujitoa serikali Zanzibar
Habari za SiasaTangulizi

ACT -Wazalendo watishia kujitoa serikali Zanzibar

Spread the love

CHAMA  cha ACT Wazalendo kimetangaza nia ya kujitoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 8 Machi 2024  jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema viongozi wa chama hicho watakutana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenzake wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussen Mwinyi kwa ajili ya kuwaeleza nia kujitoa kwenye serikali hiyo.

Ado amesema makubaliano yaliyofanywa kati ya Hayati Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Zanzibar, Dk. Mwinyi hayajatekelezwa.

Amesema moja ya makubaliano kati Maalim Seif na Dk. Mwinyi ni kurekebisho mifumo ya kiuchaguzi katika nchi ya Zanzibar ili kupatikane uchaguzi wa huru na haki na kuepusha machafuko yanayotokea katika kila uchaguzi visiwani humo.

Amesema Serikali ya SUK ni zao la umwagikaji damu za wananchi wa Zanzibar katika vipindi vyote vya uchaguzi.

“Tuliingia kwenye serikali ya umoja wa Kitaifa kwa sababu mbili ya kwanza hilo ni takwa la kisheria pili kwa sababu ya makubaliano ya Maalim Seif na Dk. Mwinyi,” amesema.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Zanzibar, inaundwa na CCM pamoja na ACT Wazalendo kupitia Mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!