Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mlezi vyuo vikuu akemea mapenzi ya jinsia moja
Habari Mchanganyiko

Mlezi vyuo vikuu akemea mapenzi ya jinsia moja

Spread the love

MJUMBE wa Kamati kuu CCM ambaye pia ni Mlezi wa vyuo na vyuo vikuu Tanzania, Dk. Frank Hawassi amewataka vijana kuheshimu agizo la Mwenyezi Mungu kwa kujiweka kando na wimbi la mapenzi ya jinsia moja kwani wale wanaofanya ni laana na machukizo mbele ya Mungu.

Pia amewaasa vijana hao kuzingatia maadili ya matumizi ya mitandao ya kijamii na kuacha kutunaka viongozi na kubeza kazi zinazofanywa na Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Hawassi ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Februari 2023 jijini Dodoma katika mkutano ambao Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na viongozi wa Jumuiya wa Wanafunzi wa Elimu ya juu (TAHLISO) na Zanzibar ZAHLIFE).

Dk. Frank Hawassi

Akizungumzia suala la maadili na ustawi wa Taifa, amesema sasa hivi kuna wimbi ambalo linaendelea ndani ya Taifa, hususani mapenzi ya jinsia moja.

Amesema jambo hilo katika vitabu vyote vya Mungu limekataliwa na hata kama wanadai kuna usawa wa kibinadamu au haki za kibinadamu, pia inabidi kuwe na haki ya Mungu.

“Kwa sababu kama Mungu amekataa jambo hili na sisi tunaendelea kulifanya kwa maana nyingine tunatengeneza Taifa ambalo linakuwa laana mbele za Mungu, familia zenye laana mbele za Mungu…hata wewe mwenyewe unakuwa na laana mbele za Mungu kwa wale wanaofanya.

“Kwa sababu ukisoma katika maandiko matakatifu yanasema mtu mume asilale na mume kama anavyolala na mwanamke, na mtu anayefanya hivi wote ni machukizo mbele za Mungu na wote wauawe na damu yao itakuwa juu yao, kwa hiyo ni agizo la Mungu naomba sana tulizingatie tulipiganie ili nchi yetu iweze kuwa salama,” amesema.

Amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kuitetea nchini kwa masilahi mapana ya Taifa.

Pia amesema kuna shida kubwa ya uwajibikaji na uadilifu miongoni mwa vijana.

“Hebu angalia sisimizi hana akida, msimamizi na mkuu anayemfuatilia, lakini pamoja na kutokuwa na msimamizi anakuwa na maarifa ya jambo lolote, anaweka chakula wakati wa jua, anakusanya wakati wa mavuno, lipo tatizo la vijana kutowajibikaji,” amesema na kuwataka vijana kutambua kuwa Tanzania inawategemea kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kamati Kuu Chadema kuketi Mei 11

Spread the loveKAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inatarajiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

error: Content is protected !!