Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mashine Bwawa la Nyerere kuwashwa Septemba
Habari Mchanganyiko

Mashine Bwawa la Nyerere kuwashwa Septemba

Bwawa la Nyerere
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na mwenendo wa ujazaji maji kwenye Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere, ifikapo katikati yam waka huu au Septemba, mashine za kuzalisha umeme huo utokanao na maji zitawashwa kwa majaribio. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema kuwashwa kwa mitambo hiyo kusaidia kumaliza tatizo la uhaba wa umeme ambao sasa unakatika kila mara.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Februari 2023 wakati akizungumza na viongozi wa Jumuiya wa Wanafunzi wa Elimu ya juu (TAHLISO), jijini Dodoma.

Amesema Serikali imejipanga vema kuhakikisha umeme unatulia na wanakwenda kusambaza nishati kwa ajili ya viwanda na wafanyabiashara wadogo na kaya zetu.

“Wote tunajua tuna mradi wa bwawa la mradi la Nyerere, naletewa picha kila baada ya wiki mbili, maji yanaingia kwa wingi, pengine katikati ya mwaka huu au Septemba tunaweza kuwasha mashine kwa majaribio,” amesema.

Amesema Tanzania inakwenda kuzalisha mbali ya umeme uliopo sasa wa zaidi ya megawati 4000 kwani zinakwenda kuongezwa 2,115.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kamati Kuu Chadema kuketi Mei 11

Spread the loveKAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inatarajiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

error: Content is protected !!