Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa AAFP wapuliza kipyenga mikutano ya hadhara
Habari za Siasa

AAFP wapuliza kipyenga mikutano ya hadhara

Spread the love

CHAMA cha Wakulima nchini (AAFP), kimetangaza mpango wa kuanza kufanya mikutano ya hadhara kuanzia Februari 2023, baada ya kufanya mkutano wake mkuu kesho Jumapili, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 11 Februari 2023 na Mwenyekiti wa AAFP Taifa, Said Sudi Said, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kwenye Uchaguzi wa Jukwaa la Wanawake na Vijana la chama hicho.

“Mikutano ya hadhara ni haki yetu, chama kinategemea kuanza mikutano lakini katika mazingira ya uadilifu sababu sio sehemu ya kufanya fujo, bali ni sehemu ya kufanya maendeleo na kueleza ushauri wetu juu ya namna gani ya kupata yale tunayohitaji. Katika demokrasia huwezi sema kiongozi hafai sababu unayotaka hayatekelezwi unapaswa kuyaeleza ili yatekelezwe,” amesema Said.

Said amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara, huku akiusifu uongozi kwamba umekuwa chachu Kwa wanawake nchini katika kufikia nafasi za juu za uongozi wa nchi.

Akizungumzia uchaguzi huo, Said amewataka wajumbe kuchagua viongozi imara watakaonisaidia chama hicho kupata matokeo mazuri katika chaguzi zijazo.

Naye Kaimu Makamu Mwenyekiti wa AAFP Taifa, Nancy Mrikaria, amewataka viongozi wa jukwaa la wanawake watakaochaguliwa wahakikishe wanakiinarisha chama ili kipate wanachama wengi zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!