Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Miswada sheria za uchaguzi zamuibua Prof. Lipumba, alilia katiba mpya
Habari za Siasa

Miswada sheria za uchaguzi zamuibua Prof. Lipumba, alilia katiba mpya

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF), ameitaka Serikali kupeleka muswada wa mabadiliko madogo ya katiba ili kupata tume huru ya uchaguzi kabla ya chaguzi zijazo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo leo tarehe 31 Disemba 2023, akitoa salamu za CUF za kukaribisha mwaka mpya wa 2024.

Prof. Lipumba amesema “Hakuna muswada wa mabadiliko madogo ya Katiba yaliyopendekezaa toka 2014 ili kuingiza uwepo wa tume huru ya uchaguzi na mgombea huru na uchaguzi wa Rais kuhojiwa mahakamani.”

“Natoa wito kwa serikali ya Rais Samia kupeleka muswada wa mabadiliko madogo ya katiba na kurekebisha muswada wa Tume ya Uchaguzi iwe Tume Huru kama ilivyopendekezwa na Mkutano wa Wadau wa tarehe 22-23 Agosti 2023. Ninawatakia Watanzania wote kheri ya mwaka mpya 2024,” amesema Prof. Lipumba.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, amesema ni vyema Serikali ikapeleka muswada wa marekebisho madogo ya Katiba, akidai miswada ya kurekebisha sheria za  uchaguzi iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma, Novemba 2023 mapendekezo yake hayatatatua matatizo yaliyojitokeza kwenye chaguzi zilizopita.

Aidha, Prof. Lipumba ameishauri Serikali kuelekea 2024 iweke mikakati ya kutatua changamoto zilizowakabili wananchi 2023, ikiwemo mgawo wa umeme na kupanda gharama za maisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!