September 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Michezo mwezi Oktoba, Simba ni jasho na damu

Spread the love

 

IKIWA kawa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara, imesimama kwa baadhi ya timu ili kupisha michezo ya kimataifa kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), klabu ya Simba itakuwa na kazi ngumu endapo Ligi hiyo itarejea mwezi Oktoba mwaka huu. Anaripoti Damas Ndelema…(endelea)

Licha ya michezo ya Ligi, katika mwezio huo oktoba, Simba itakuwqa na michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa mzunguko wa kwanza dhidi ya Premio De Agosto ya nchini Angola.

Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na klabu hiyo mchezo wa kwanza, utapigwa tarehe 9 Oktoba 2022, nchini Angola na mchezo wa marudiano utapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam tarehe 16 Oktoba 2022.

Kwenye ratiba ya Ligi inaonesha kwenye mwezi huo Oktoba kabla ya kukutana na mtani wake klabu ya Yanga kwenye mchezo utakaopiugwa Oktroba 23, 2022 Simba wataanza kumenyana kwanza na Singida Big Stars kwenye mchezo wa ugenini mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Liti mkoani Singida, tarehe 12 Oktoba 2022.

Mara baada ya kumenyana dhidi ya Yanga, Simba itaumana tena dhidi ya Azam FC, ambayo kwa sasa imeonekana kuimalika kutokana na aina bya usajili walioufanya, na ratiba ya mwezi huo kwa Simba itakamilika kwa kushuka dimbani dhidi ya Mtibwa Sugar kutoka Manungu Morogoro.

Mpaka sasa Simba imeshacheza jumla ya michezo minne, ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo nyuma ya Yanga ambao wanaongoza msimamo huo wote wakiwa na alama 10 wakitofautiana kwenye mabao ya kufunga, ambapo Simba wamefunga mabao nane, na Ysanga wamefunga mabao tisa.

error: Content is protected !!