Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari Mgombea urais aahidi kutoa mkopo kwa wanandoa wapya
Habari

Mgombea urais aahidi kutoa mkopo kwa wanandoa wapya

Spread the love

 

Mgombea urais nchini Kenya ameahidi mikopo ya kati ya Dola za Marekani 4,400 (Sh milioni 10.1) na 8,800 (Sh milioni 20.20) kwa wanandoa wote wapya iwapo atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mkuu mwakani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Gavana wa Machakos Alfred Mutua, ambaye alikuwa akizindua ilani yake ya urais jana tarehe 5 Disemba, 2021 alisema mkopo wa riba ya chini utakaolipwa ndani ya miaka 20 utasaidia familia kuanza maisha vizuri.

Vilevile mgombea huyo amesema serikali yake itahimiza upandaji miti ambayo itahesabiwa kama sehemu ya malipo ya mahari.

“Unapoenda kulipa mahari, unapaswa kusema umepanda miti mingapi,” Mutua alisema wakati wa uzinduzi huo ambao ulitangazwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni nchini humo.

Lakini ahadi hii imeibua shutuma nzito na kejeli kutoka kwa Wakenya mtandaoni.

Takriban wanasiasa 12 tayari wameanza kampeni za kumrithi Rais aliye madarakani Uhuru Kenyatta, ambaye yuko katika miezi ya mwisho ya miaka 10 madarakani.

Miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo ni kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga na Naibu Rais wa sasa William Ruto, ambao wanaonekana kuwa wagombea wakuu katika uchaguzi wa Agosti 2022.

Uchumi, ukosefu wa ajira kwa vijana na kupambana na ufisadi vimeibuka kuwa masuala muhimu katika ajenda za wanaowania urais, lakini chaguzi zilizopita zimeonesha kuwa Wakenya wengi hupiga kura kwa kuzingatia ukabila badala ya masuala ya sera.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!