May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rekodi ya kipee kwa mwamuzi Herry Sasii mchezo wa Simba na Yanga

Spread the love

 

BODI ya Ligi kupitia kamati ya waamuzi, imemchagua Herry Sasii kuwa refa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaowakutanisha vigogo wa soka nchini Simba na Yanga. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Herry Sasii unakwenda kuwa mchezo wake wa tatu wa watani wa jadi, huku katika michezo miwili aliyochezesha hakuna timu iliyofanikiwa kuibuka na matokeo ya ushindi ndani ya dakika 90 ya mchezo.

Mchezo huo utapigwa Jumamosi ya tarehe 11 Disemba, 2021 majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mwamuzi huyo alichezesha mechi yake ya kwanza ya watani wa jadi Agosti 2017, mchezo wa ngao ya hisani kuashilia ufunguiz wa Ligi kwa msimu wa 2017/18, ambapo ndani ya dakika 90 mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya kutofungana na Simba alitwaa ngao hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya Penati (5-4).

Mara baada ya kuonekana kumudu vizuri pambano hilo, mwamuzi huyo alipewa tena dhamana kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye msimu huo huo, uliopigwa Oktoba 2017.

Katika mchezo huo Simba na Yanga zilitoshana nguvu kwa kwenda sare kwa kufungana bao 1-1, mchezo uliopigwa kwenye dimba la uhuru.

Bao la Simba kwenye mchezo huo liliwekwa kambani na Shiza Kichuya, huku bao la kusawazisha la Yanga lilifungwa na Obrey Chirwa.

Mchezo wa jumamoso utakuwa wa tatu kwa mwamuzi huyo mwenye beji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), huku akisaidiwa na Kassim Mpangakutoka Dar na Hamdani Saidi kutoka Mtwara, huku mwamuzi wa akiba akiwa Ahmada Simba wa Kagera.

error: Content is protected !!