Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee, wenzake wafika mahakamani, kesi yaanza kunguruma
Habari za SiasaTangulizi

Mdee, wenzake wafika mahakamani, kesi yaanza kunguruma

Spread the love

 

KWA mara ya kwanza Halima Mdee na wenzake sita, ambao ni Wabunge wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama wa Chadema, wamefika mahakamani kuitika wito wa mahakama. Anaripoti Faki Sosi na Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).

Awali tarehe 29 Julai mwaka huu Mahakama hiyo ilikubali ombi la Mawakili wa Chadema lililowasilishwa na Peter Kibatala la kutaka waombaji saba kwenye kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, kufika mahakamani hapo.

Mdee na wenzake wameomba mahakama hiyo kutengua kuvuliwa kwa uanachama wao ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Shauri hilo limeanza kusikilizwa saa tano kamili ambapo Jaji Cyprian Mkeha ameanza kusikiliza pingamizi la upande wa waombaji .

Pingamizi hilo limewasilishwa kupinga kiapo kinzani cha upande wa wajibu maombi namba moja (Chadema).

Endelea kusoma MwanaHALISI Online kujua zaidi kinachoendelea mahakamani hapo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!