Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mchungaji Mackenzie afanya vurugu mahakamani
Kimataifa

Mchungaji Mackenzie afanya vurugu mahakamani

Spread the love

MCHUNGAJI Paul Mackenzie na washtakiwa wenzake 29 wamesababisha vurugu katika Mahakama ya Shanzu wakipinga ombi la upande wa mashtaka kwa mahakama kutaka watuhumiwa wazuiliwe kwa siku 47 zaidi. Anaripoti Isaya Temu, TURDARco … (endelea).

Watuhumiwa hao walipinga ombi hilo baada ya wapelelezi upande wa serikali kutaka muda zaidi ili kukamilisha uchunguzi wao kabla ya kuanza kusikiliza kesi dhidi ya watuhumiwa hao.

Mackenzie ambaye analiongoza kanisa la Good News International na wenzake wanashikiliwa kwa makosa ya kuendesha shughuli za kishirikina ambapo watu wengi walifariki, baada ya kuwaaminisha waumini wake kuwa wakifunga wataweza kukutana na Mungu.

Mchungaji huyo na wenzake 29 walipinga ombi hilo la serikali kwa kuanza kuimba nyimbo zilizokuwa zinamaanisha kudai haki yao hali iliyoleta sintofahamu mahakamani hapo.

Pia walikemea vitendo wanavyofanyiwa ambazo si vya kibinadamu kwa kuzuiliwa ndani pamoja na kulazimishwa kuvaa nguo za magereza licha ya kutokuwa na hatia, kulazimishwa kuwekwa safu, kulala chini na kujisaidia ndani ya ndoo.

Baada sintofahamu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Yusuf Shikanda aliagiza watuhumiwa hao kuendelea kushikiliwa kwa siku mbili zaidi kabla ya mahakama kutoa uamuzi kuhusu maombi ya upande wa mashtaka.

Hayo yanatokea baada ya kundulika makaburi kadhaa ya kina kirefu katika eneo kubwa la msitu wa Shakahola katika kaunti ya Kilifi ambapo kulikutwa miili kutoka makaburini inasadikiwa ilikuwa ya wafuasi wa Mackenzie ambao walikufa njaa iliyosababishwa na kufunga kwa muda mrefu.

Mganga Mkuu wa Serikali ya Kenya tangu wakati huo amekuwa akiendesha uchunguzi kwa kufanya upasuaji kwenye miili iliyopatikana.

Mwezi Juni mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Kenya, Kithure Kindiki alisema msitu wa Shakahola hautabaki kama ulivyokuwa baada ya zoezi la kuteketeza.

“Serikali itaugeuza kuwa kumbukumbu ya kitaifa, mahali pa kumbukumbu ili Wakenya na ulimwengu usisahau kilichotokea hapa,” alisema waziri huyo.

Kwa mujibu wa Kindiki, mara baada ya zoezi hili kukamilika, serikali itaita mkusanyiko wa waumini wote kutoka dini zote na uongozi wa kitaifa kwa ajili ya ibada ya maadhimisho.

“Maombi hayo yatalenga kulinda haki takatifu na uhuru wa kuabudu ambao umekiukwa na wadanganyifu wanaojificha nyuma ya maandiko,” aliongeza waziri Kindiki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!