Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Infinix Note 30 yajizolea sifa kimataifa mwaka 2023
Biashara

Infinix Note 30 yajizolea sifa kimataifa mwaka 2023

Spread the love

 

CHAPA ya simu mahiri inayoongoza kwa ubora  Infinix Mobile LTD imegonga vichwa vya habari wiki hii baada ya Infinix NOTE 30 kushinda tuzo ya Usanifu wa bidhaa/Vyombo vya habari na Tuzo ya Electroniki za nyumbani zinazoandaliwa kwa kila Mwaka nchini Paris. NOTE 30 imeundwa kukidhi mahitaji ya mitandao ya simu za mkononi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tuzo za Paris Design hutoa heshima katika taaluma ya Usanifu, Usanifu wa Ndani, Usanifu wa Mandhari, Usanifu wa Picha na Usanifu wa Bidhaa ikitunuku mbunifu bora zaidi duniani kote.

Hii ni heshima kubwa kampuni hii ambayo inakuwa kwa kasi kubwa inayotokana na uzalishaji wa bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa gharama nafuu. Tanzania ni moja ya nchi ambayo inanufaika vyema na bidhaa za kampuni hiyo, imekuwa na mchango mkubwa katika kufanya teknolojia ya mawasiliano kupitia njia ya simu kuenea kwa wepesi.

Kufuatia ushindi wa Tuzo hii ya bidhaa yenye muundo mzuri kwa mwaka 2023 Infinix Tanzania kufuatia kurasa zake za mitandao ya kijamii imetupia video na jumbe ya kujipongeza na kuwataka wadau wa Infinix kujivunia Chapa hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa kampuni hii kushinda Tuzo hizo za kimataifa Mwaka 2021 pia ilitwaa Tuzo ya bidhaa yenye nidhamu katika kitengo cha mawasiliano huko barani Asia. Pongezi nyingi kwao na kwa mashabiki wa chapa hii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!