Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia leo Jumatano, tarehe 2 Agosti 2023 saa 6:01 usiku huku zikiwa zimepanda ikilinganishwa na bei za mwezi uliopita. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mikoa ya Dar es Salaam ni kama ifuatavyo kwa lita: Petroli 3,199, Dizeli 2,935 na mafuta ya Taa 2,668.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa leo Jumatano, mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yanatokana na changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani na mabadiliko ya sera za kikodi.
Pia kupanda kwa mafuta hayo kumesababishwa na kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.
Leave a comment