Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea
Habari Mchanganyiko

Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea

Spread the love

MAWASILIANO ya barabara ya Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, kupitia Bagamoyo, yaliyokuwa yamefungwa baada ya sehemu ya Daraja la Mto Mpiji kumomonyoka uliosabaishwa na mvua za El-Nino, yamerejeshwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano cha Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mawasiliano hayo yamerejeshwa asubuhi ya leo tarehe 9 Disemba 2023, baada ya barabara hiyo kufungwa jioni ya jana Ijumaa.

Taarifa ya wakala huo ilisema, daraja hilo lilifungwa kwa ajili ya usalama wa wasafiri na kwamba limefunguliwa baada ya watalaamu wake kufanya jitihada za kutengeneza hitilafu iliyojitokeza.

“TANROADS imerejesha mawasiliano ya barabara ya mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, kupitia Bagamoyo baada ya daraja la Mpiji linalounganisha mikoa hiyo kupata changamoto ya kumomonyoka kutokana namvua za El-Nino,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“TANROADS imeruhusu watumiaji wa barabara hiyo kupita upande mmoja wa daraja baada ya matengenezo kukamilika, huku timu ya watalaamu na mkandarasi wakiendelea kufanya matengenezo mengine ya haraka kulirejesha kwenye hali yake ya awali na kulifanya liweze kuwa na uimara zaidi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!