Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira mpya ya taifa ya maendeleo (2025 hadi 2050), huku akitaka iweke masuala yatakayosaidia kujenga jamii yenye ujasiri wa kuhoji watumishi wa umma wanaojipatia mali kinyume cha sheria (mafisadi). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Agizo hilo la Rais Samia amelitoa leo tarehe 9 Disemba 2023 jijini Dodoma, akizungumza kwenye mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 20250, pamoja na maadhimisho ya sherehe za miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Mkuu huyo wa nchi ametoa agizo hilo wakati akizungumzia mafanikio ya dira ya taifa inayomaliza muda wake, katika uimarishaji maadili ya taifa, ambapo amesema katika suala hilo nchi imepiga hatua kubwa kwa kuweka mifumo ya kuongeza uwazi na kusimamia maadili ya utumishi wa umma.

“Tathmini iantuonyesha tumepiga hatua kwa kuongeza uwazi, kusimamia maadili ya utumishi wa umma na hili tutaendelea kulisimamia vyema lakini inabidi twende mbali zaidi, lazima tuwe na jamii yenye ujasiri wa kuhoji wanaojipatia mali wasio na maelezo nazo,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “lazima tuwe na jamii inayopinga rushwa kila mahali, jamii inayoweza kujituma na kufanya kazi bila kusukumwa, jamii ambayo haiwaibii waathiriwa wa ajali badala ya kuwaokoa. Tujenge jamii ya watu mahiri, makjini na waadilifu. Bila shaka suala hili litapewa uzito mkubwa kwenye majadala wa kuandaa sira mpya.”

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameiagiza kamati inayoratibu maandalizi ya dira hiyo, kuhakikisha inaweka mazingira yatakatoongeza mchango wa mashirika ya umma, sekta binafsi za ndani na nje ya nchi kwenye ukuzaji uchumi.

Pia, ameagiza dira hiyo iweke mazingira yatakayofungamanisha miradi ya vipaumbele kwa sekta za uzalishaji pamoja na kuchochea ukuaji uchumi kwenye maeneo yanayogusa wananchi moja kwa moja na kuwatengeneza ajira.

“Dira mpya itakayoandikwa itiliwe maanani ukweli kwamba dunia inakabiliwa na uhaba wa kutokuwa na usalama wa chakula, matarajio ya dira inayoandikwa ni kuweka lengo la kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji chakula kwa ajili ya Afrika. Kuna haja kuongeza hadhi ya elimu inatolewa,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!