Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma
Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the love

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini kuhakikisha suala la kukatika kwa umeme linashughulikiwa kikamilifu na hakuna hujuma yeyote kama ambavyo inasemekana. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo jana tarehe 8 Desemba 2023 wakati akijibu swali ya mwananchi wa Kijiji cha Masimba, Kata ya Tongwe wilayani Muheza kuhusu kukatika kwa umeme huo kijijini hapo.

“Ninakubaliana na yeye kuwa umeme unakatika kwa kuwa tunapitia kipindi cha mgawo wa umeme, lakini niwahakikishie ndugu zangu, Mheshimiwa Rais alitupatia miezi sita kuhakikisha tunaondoa mgao wa umeme.

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

“Tupo kazini na kwa mipango ambayo tunayo tunategemea ndani ya miezi sita hiyo tutakuwa tumeshaondoa mgawo wa umeme, miezi sita inaisha mwezi wa tatu 2024, mpaka kufikia hapo na kwa mipango iliyopo miradi ambayo Rais ametupatia fedha tunatekeleza tunategemea tutaondoka kabisa kwenye mgao wa umeme,” amesema na kuongeza;

“Kwa kipindi hiki mvua zinanyesha, maeneo kwa maeneo, maeneo ambayo tunafanya uzalishaji wa umeme kule kwenye mabwawa yetu ya umeme Kidatu, Kihansi na Mtera ndio mvua zimeanza kwa hiyo tunategemea kadiri mvua zinavyoendelea kunyesha, maji yanavyoendelea kujaa tutakuwa tumepunguza tatizo kwa kiasi kikubwa.

“Hivyo niwaondoe shaka, hakuna hujuma inayofanyika kama ambavyo  inasemwa watu wanauza majenereta, sola hapana… Serikali ipo kazini na tunaangaliza jicho kwelikweli,” alisema Naibu Waziri Kapinga.

Aidha, amebainisha lengo la Serikali ni kuhakikisha inatoa huduma bora na stahiki ya upatikanaji wa umeme ambao ni wa kudumu na utawasaidia wananchi kwenye shughuli za maendeleo.

Mbali na hayo, Kapinga amewasihi wananchi kuendelea kuunganisha umeme kwenye majumba yao ili miradi hiyo ikifika, waweze kuunganishwa na kuona thamani ya miradi ambayo inapelekwa kwenye vitongoji na vijiji hivyo.

Hata hivyo, Kapinga amewaahidi wakazi wa Kijiji cha Masimba kumaliza suala la usambazaji wa umeme katika vitongoji viwili vilivyobaki katika Kijiji hicho.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika Jimbo la Muheza ili kuboresha huduma za jamii.

Jimbo hilo lina jumla ya kata 37, vijiji 135 na vitongoji 522, hata hivyo vijiji vyote 135 vimepatiwa huduma ya umeme kupitia mradi wa awali wa REA III (Mzunguko wa Kwanza na wa Pili) na PERI Urbani III.

1 Comment

  • Duh!
    Umeme ukikatika katika kwenye nchi yeyote ya Ulaya basi watu watatupa nyama za frijini kwa waziri, naibu waziri, na bosi wa Tanesco.
    Kwa nini JN Hydroelectric Power Plant haijaanza kwa wakati….hujuma?
    Acheni kumsingizia Mama, hiyo ni wizara yako. Akutumbue tu?
    Ili tuendelee, tunahitaji ujasiri wa kufukuza wavivu na mangi meza.
    Mbona umeme ulikuwa haukatiki ovyo ovyo wakati marehemu Salvatory Mosha alipokuwa mkuu wa Tanesco?
    Au ni hujuma za kuuza majenereta?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!