Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Balozi Mwamweta awasilisha hati za utambulisho kwa Rais Ujerumani
Habari za Siasa

Balozi Mwamweta awasilisha hati za utambulisho kwa Rais Ujerumani

Spread the love

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Hassan Iddi Mwamweta amewasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Frank Walter Steinmeier katika Ikulu ya Nchi hiyo jijini Berlin. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hati hizo Rais Steinmeier alifafanua kuwa Serikali yake inaunga mkono jitihada za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Tanzania na Ujerumani zinashirikiana kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, utunzaji wa mazingira, utamaduni, uhifadhi wa mazingira, utalii, biashara, uwekezaji pamoja na kubidhaisha kiswahili.

Itakumbukwa pia katika jitihada za kuimarisha ushirikiano Steinmeier alifanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania kuanzia tarehe 30 Oktoba mpaka tarehe 1 Novemba 2023 akiwa ameambatana na ujumbe wa kampuni mbalimbali kwa ajili ya kuangalia fursa ili kuwekeza nchini.

Pamoja na ratiba nyingine akiwa nchini alifanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia ambapo mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuendeleza na kukuza ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kwa maslahi ya pande zote mbili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!