Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na vikosi vya Hamas yameanza leo Ijumaa saa moja asubuhi ikiwa ni mpango wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku nne. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).
Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar, ambayo inasaidia kujadili muafaka wa mapigano hayo, kundi la kwanza la mateka linatarajiwa kuachiliwa kutoka Gaza saa kumi jioni.
Msemaji huyo Majed Al-Ansari, aliwaambia waandishi wa habari jijini Doha kwamba usitishaji huo wa kwanza tangu vita kuanza mwezi uliopita utajumuisha usitishaji vita wa pande zote kaskazini na kusini mwa Gaza.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, wanawake na watoto 50 waliotekwa nyara kutoka Israel, na kundi la wanamgambo wa Hamas tarehe 7 Oktoba, 2023 wataachiliwa kwa kubadilishana na wanawake 150 wa Kipalestina na watoto wadogo waliofungwa gerezani nchini Israel.
Mateka 13 wataachiliwa kutoka Gaza leo saa 10 jioni na makundi mengine ya mateka yataachiliwa kila siku ya kusitisha mapigano hadi 50 waachiliwe.
Leave a comment