Takriban watu 573 kati ya 11,640 walioambukizwa kipindupindu nchini Nigeria wamepoteza maisha tangu mlipuko wa ugonjwa huo uanze Desemba 2022. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Hata hivyo, maofisa wa masuala ya afya wanakadiria kuwa idadi hiyo kwa sasa inapungua kwa sababu ya juhudi za matibabu katika majimbo ambayo hayawezi kugundua maambukizo mengi.
Serikali kadhaa za Afrika magharibi zinajaribu kudhibiti mlipuko huo wa kipindupindu, ikiwa ni pamoja na Nigeria ambapo afisa wa ngazi ya juu wa afya jana Alhamisi amesema kwamba mamilioni ya watu wanapewa chanjo ili kufidia kinga dhidi ya ugonjwa huo.
Nchini Niger, watu 37 wamefariki dunia katika kesi 865 kufikia Oktoba mwaka huu, wakati Guinea imeripoti vifo 58 kati ya maambukizi 497 tangu kuzuka kwake mwezi Juni mwaka huu.
Maambukizi hayo ya bakteria yanayosambaa kwa kasi yameripotiwa katika majimbo 20 kati ya 36 ya Nigeria mpaka hivi sasa.
Leave a comment